Best 802 of Enock Maregesi quotes - MyQuotes

Follow
Enock Maregesi
By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ukila chakula mwili wote unafaidi! Ukiomba kitu kwa Mungu omba kwa ajili ya wote.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ukiogopa kushindwa hutashinda.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Murphy hakupenda kupoteza muda. Alinyanyuka na kumimina risasi, Mungu akamsaidia akadondosha wawili huku wengine wakipotea kwa kuruka vibaya na kukwepa. Kwa kasi Murphy alikimbia huku ameinama mpaka katika milango mikubwa ya nje, ambayo sasa ilikuwa wazi. Hapo akasita. Chochote kingeweza kumpata kwa nje kama hangekuwa mwangalifu. Bunduki yake ilishakwisha risasi. Aliitupa na kuchungulia nje akaona adui mmoja akikatisha kwenda nyuma ambako ndiko mashambulizi yalikokuwa yakisikika sasa. Murphy hakumtaka huyo. Aligeukia ndani kuona kama kulikuwa na bunduki aichukue lakini hata kisu hakikuwepo. Akiwa bado anashangaa, ghafla alitokea adui – kwa ndani – na kurusha risasi, bahati nzuri akamkosa Murphy. Murphy, kama mbayuwayu, aliruka na kusafiri hewani hapohapo akadondoka nyuma ya tangi la gesi karibu na milango ya nje. Alipoona vile, adui alidhani Murphy alidondoka mbali. Alibung’aa asijue la kufanya. Wasiwasi ulipomzidi alishindwa kuvumilia. Alishika bunduki kwa nguvu na kupiga kelele, "Yuko hukuuu!" Halafu akajificha ili Murphy asimwone. Lakini Murphy alikuwa akimwona.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Mheshimu yule ambaye ni mkubwa au mdogo kwako hata kwa siku moja.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Usikate tamaa kabla ya kufa. Pambana.

By Anonym 18 Sep

Enock Maregesi

Soma sana. Andika sana. Ongea na watu kuhusu mambo ya muhimu unayoyafikiria. Tumia intaneti na maktaba kwa makini kwa ajili ya utafiti, kwa sababu habari nyingi za intaneti na maktaba haziaminiki. Kama una wazo kichwani mwako lizungumze kwa watu kama mazungumzo ya kawaida, ili upate maoni yao ya dhati, bila kusahau kuandika kwa siri wazo lolote jipya utakalolipata kutokana na mazungumzo hayo. Maana Mungu anaweza kuwasiliana na mtu mwingine yeyote yule akupe wazo, litakaloongeza maana zaidi katika mawazo ambayo tayari unayo.

By Anonym 18 Sep

Enock Maregesi

Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ujanja wote ulimwisha Murphy. Ilimbidi kutoboa siri ili adui asizidi kumuumiza. Alilaumu mno kufa wakati alishakula ng’ombe mzima. Alifikiri Mogens na Yehuda walishauwawa kulingana na hasira nyingi za magaidi. Walihakikisha hawafanyi makosa hata kidogo. Alivyomaliza kumhoji, yule adui alizunguka nyuma katika mgongo wa Murphy na kwenda katika dirisha lililokuwa wazi – la mashariki – ambapo aliegemea na kuvuta sigara. Alichungulia kidogo nje kisha akageuka na kuendelea kupata upepo mdogo wa baridi.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Geuza hasira yako kuwa hekima.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ukarimu ni bora kuliko hekima, na kulitambua hilo ndiyo mwanzo wa hekima.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Live as you were created to live.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Wananchi wanapokosa huduma za muhimu za kijamii (kama vile afya, elimu, chakula, malazi, na ulinzi) ilhali wanalipa kodi, na wameajiri serikali kuwaendeshea nchi kwa kiapo cha uaminifu wa vitabu vitakatifu, watakosa imani na serikali yao! Vilevile wataathirika kiuchumi, kijamii na kisiasa, na vita itaweza kutokea kati ya wananchi na serikali, au wananchi kwa wananchi wataweza hata kujidhuru wenyewe – nikimaanisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Serikali ikifuata maadili ya kazi, na kuacha udikteta na urasimu wa aina yoyote ile, au ikifanya kazi kulingana na misingi ya katiba ya nchi; wananchi watapata huduma za kijamii kama wanavyostahili, na ndoto ya haki na ustawi wa jamii itaweza kutimia. Hata hivyo, serikali inaweza kuwadhulumu wananchi wake kwa sababu ya usalama wao.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Kolonia Santita ilikuwa na tani 627.54 za madawa ya kulevya ilizokuwa imezikusanya kwa siri kwa muda wa miezi 9 mfululizo. Ilikuwa imepanga kuzisafirisha ndani ya siku 10 baada ya kutokea kwa mauaji ya Tijuana-San Diego, katika mpaka wa Meksiko na Marekani; kwenda Asia, Afrika, Amerika, Ulaya na Australia, kabla ya kukamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani WODEA. Kokeini tani 183, heroini tani 90, methamfetamini tani 81, eksitasi tani 27.54 (vidonge milioni 110.16). Bangi tani 186, uyoga wa kichawi tani 60. Madawa hayo yalikuwa na thamani ya mtaani ya shilingi za Kitanzania trilioni 12.9.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.

By Anonym 20 Sep

Enock Maregesi

XM29 OICW ni bunduki iliyowasaidia Vijana wa Tume kubomoa jengo la utawala la Kolonia Santita katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals jijini Mexico City, iliyowasaidia kukamata baadhi ya wakurugenzi wa Kolonia Santita kabla hawajatoroshwa na walinzi wao makomandoo. Bunduki hii inayotumia teknolojia ya OICW ('Objective Individual Combat Weapon') iliyotengenezwa na Kiwanda cha Heckler & Koch cha Ujerumani, ina uwezo wa kufyatua makombora ya HEAB ('High Explosive Air Bursting') yenye ukubwa wa milimeta 20; ambayo hulipuka hewani kabla ya kugonga shabaha, kwa lengo la kusambaza vyuma vya moto katika eneo lote walipojificha maadui. Bunduki hizi hazitumiki tena. Zilitumika mara ya mwisho mwaka 2004.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Nukuu ya mwandishi wa vitabu wa Brazili, Paulo Coelho, "Tunapopenda tunajitahidi siku zote kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo. Tunapojitahidi kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo, kila kitu katika maisha yetu kinakuwa kizuri hali kadhalika.", inadhihirisha kikamilifu tabia ambayo bibi yangu (Martha Maregesi) alijitahidi kuwa nayo katika kipindi cha maisha yake yote. Alikuwa mtu mwenye furaha sana. Alikuwa na tabasamu lenye kuambukiza ambalo marafiki na familia yake hawakuweza kujizuia kutabasamu pia alipofurahi nao. Pamoja na kwamba alikumbana na matatizo mengi na bahati mbaya nyingi katika maisha yake, alijulikana kama mtu mwenye upendo na uvumilivu mkubwa.

By Anonym 20 Sep

Enock Maregesi

WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Mwenye hekima huzungumza kilicho na maana! Kinaweza kuwa kizuri au kibaya.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Wachawi hawamwabudu Shetani kwa sababu dhana ya Shetani ni dhana ya Kikristo, na wachawi si Wakristo.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Hatumtaki kiongozi anayeishi katika mifuko ya mafisadi, tunamtaka kiongozi anayeishi katika ibara za katiba ya nchi. Kitambi bila Yesu ni jipu.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ukiwa na mawazo ya watu 8 unakuwa 1/8 ya mawazo yao.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Mwendawazimu anaweza kuzungumza jambo la maana, kwa maana ya kuongozwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, usimdharau mtu. Kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Hakuna kocha wa maisha kama Yesu Kristo. Swali ni je, unakochika?

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Kwa mfano, uko kwenye mashindano ya mbio za mita 100. Utakapofika kwenye kamba, mwisho wa hizo mita 100, utakuwa umechoka sana. Lakini kocha anakuhimiza uendelee mbele mita nyingine 50! Unaweza kufika ukiwa mzima au unaweza kufika ukiwa umezimia. Lakini usijali. Ukiendelea mita nyingine 50 utakuwa umetumia uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Ukitumia kanuni hiyo katika maisha yako ya kawaida utaweza kufanikiwa.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Wakati mwingine tukitaka kufanikiwa lazima tujifunze kutunza siri.

By Anonym 18 Sep

Enock Maregesi

Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli?

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Onesha lugha ya mwili ya kutaka kusalimia au kusalimiwa.

By Anonym 15 Sep

Enock Maregesi

Debbie alilia. Alilia kwa nguvu zake zote. Alijua tayari alishampoteza Murphy na yote yale huenda alisababisha yeye. Bila kujuana na Vijana wa Tume huenda wasingepigwa. Debbie Hakukata tamaa. Alikumbuka kitu halafu akamwita dereva. Alimwomba dereva amkimbize Roma Notre haraka ilivyowezekana. Alidhani alijua majambazi walikokuwa wakikimbilia na kuna kitu alitaka kufanya. Dereva akamkubalia na kuondoka kuelekea Roma Notre. Njiani Debbie hakuacha kulia. Aliwaza alivyompoteza Marciano, akawaza kumpoteza na Murphy. Jibu alilolipata ni kumwokoa Murphy kwa gharama yoyote ile.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Umeufanyia nini ulimwengu?

By Anonym 18 Sep

Enock Maregesi

Pesa ikitolewa kwa masharti mazuri chukua, kama masharti ya kibenki, si masharti mabaya kama ya kiganga, huyo anayeitoa si ya kwake. Pesa mbaya imebarikiwa na Shetani, ukiichukua umeingia agano na Shetani, jambo ambalo Mungu hapendi. Chukua pesa kutoka kwa mtu unayemjua ambaye hana masharti au hana masharti ya kishetani, au usiyemjua.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Unapofikia hatua ya kuwa na kila kitu katika maisha, unapokuwa umefanya kila kitu ulichotamani kufanya katika maisha, unakuwa na bahari nzima ndani ya tone ambalo ni wewe. Unaridhika. Wewe si tone tena ndani ya bahari, wewe ni bahari ndani ya tone. Kinachobaki baada ya hapo ni kusaidia jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo, kuacha alama katika dunia kabla na baada ya wewe kuondoka, bila kujali watu watasema nini juu ya maisha yako.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Uzima wa milele si mchezo wa kubahatisha! Kila mtu atalipwa kulingana na matendo yake, mema au mabaya, na huo uzima wa milele atapewa yule atakayetenda mema maisha yake yote.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Tumia kipaji ulichopewa na Mungu.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Gluttony is the act of digging a grave with your own teeth.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Maombi ya sifa huunganisha watu wa Mungu na hutayarisha njia kwa ajili ya uwezo wa Mungu katika maisha yetu. Thamani ya maombi ya sifa wakati wa matatizo ni kuimarisha imani yetu, na kuwa karibu na Mungu wetu. Mungu anataka tumpe sifa na kumshukuru kwa kila jambo, kama Mtume Paulo anavyosema katika waraka wa kwanza wa Wathesalonike 5:16-18. Kumshukuru Mungu wakati wa matatizo ni amri, si ombi.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Usipochangia mawazo wewe ni mwizi, unaiba mawazo ya wengine, wewe ni mbinafsi pia.

By Anonym 20 Sep

Enock Maregesi

Your mind wants to succeed, but your life does not want; how will you succeed? Success is not an easy thing! Success is allergic to laziness! However, it is amenable to intelligence and diligence.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Majambazi huwapenda wanaowapenda. Chukulia mfano huu: Mimi na Wanda ni marafiki, OK? Baba yake, au genge la baba yake, hataweza kunidhuru au kuwadhuru watu ninaowapenda kwa sababu tu ya urafiki na mtoto wake. Na yeye anaweza kufumbiwa macho akifanya makosa kwa sababu mimi na mtoto wake ni marafiki wakubwa. Murphy, hapa Meksiko tuna kitu kinaitwa Bima ya Utekaji Nyara ('Ransom Insurance'). Zamani nilikuwa nalipa dola milioni kumi za Marekani kama bima ya utekaji nyara; Lisa alikuwa analipa milioni nne na Wanda bado analipa milioni mbili mpaka sasa hivi. Baada ya mimi na Lisa kujenga urafiki na Wanda, malipo yetu ya bima yamepungua mpaka dola milioni moja kwa mwaka.

By Anonym 16 Sep

Enock Maregesi

Hata wamisionari, hasa wamisionari wa Kiprotestanti, hawakukitumia Kiingereza katika kueneza dini kwa sababu hadhira yao isingewaelewa. Badala yake walitumia lugha za makabila ya Kiswahili, hivyo kujikuta wakieneza zaidi utamaduni wa Kiswahili kuliko wa Kiingereza au Kijerumani.

By Anonym 19 Sep

Enock Maregesi

Usipobadilika hutapata mwenza bora wa kuoana naye.

By Anonym 17 Sep

Enock Maregesi

Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.